Quantcast
Channel: Afya – Fikra Pevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Utafiti umegundua baadhi ya Njia za Uzazi wa Mpango huongeza Hatari ya Kuambukizwa VVU

$
0
0

Njia za uzazi wa mpango zenye homoni mfano vidonge vya uzazi wa mpango (POPs & COCs), sindano za uzazi wa mpango (Depo-Provera) na vipandikizi/vijiti (Implanon) ndio njia za uzazi wa mpango zinazofanya kazi kwa ufanisi mkubwa na kutumika kwa wanawake wengi zaidi duniani.

Njia hizi za uzazi wa mpango zina faida za kiafya kutia ndani faida za uzazi wa mpango mfano kuzuia mimba na zisizo za uzazi wa mpango mfano kurekebisha mzunguko wa hedhi. Pamoja na kuwa na faida lukuki njia hizi pia zina hatari za kiafya kwa uchache kama kuongeza hatari ya kuambukizwa VVU.

Katika miaka ya hivi karibuni, ushahidi umeendelea kujengeka kuwa sindano za uzazi wa mpango za Depot medroxyprogesterone acetate (Depo-Provera au DMPA) zina uhusiano wa karibu na kuongezeka kwa hatari ya maambukizi ya VVU.

Utafiti mpya uliochapishwa katika jarida la mtandao la Jamii ya Wataalamu wa Mikrobiolojia (Sayansi inayohusu vidubini) wa Amerika liitwalo mBio, lililotoa maelezo ya kibiolojia kuhusu jambo hili. Matokeo ya utafiti huu yatasaidia wanawake kufanya uchaguzi mzuri kuhusu njia bora za uzazi wa mpango.

Mkurugenzi wa Kitengo cha Biolojia ya Sehemu za Siri katika Hospitali ya Brigham & Wanawake na Profesa wa Obstetrikia (tanzu ya tiba inayohusu mimba, kuzaa & puperiamu) na Ginakolojia (tanzu ya utabibu inayohusu magonjwa ya kike, hasa yanoyoathiri viungo vya uzazi) katika Chuo cha Tiba cha Harvard huko Boston, Marekani Dk. Raina Fichorova, alikaririwa na FikraPevu "Kabla ya utafiti huu, kumekuwepo na ripoti zenye utata, baadhi zikionyesha kwamba DMPA huongeza hatari ya kupata maambukizi ya VVU na baadhi zilipinga bila ya kuwa na maelezo mazuri ya kibiolojia kuhusu utofauti wa tafiti hizi" 

Watafiti walichunguza ute uliotolewa kwenye seviksi (mlango wa kizazi) za wanawake 823 kati ya umri wa miaka 18 na 35 ambao hawakuwa na VVU na walianzishwa Kliniki ya Uzazi wa Mpango nchini Uganda na Zimbabwe. Inakisiwa wanawake 200 kati yao walipata VVU.

Wanawake waligawanywa kwenye makundi matatu, wale waliotumia sindano za uzazi wa mpango (Depo-Provera au DMPA), wale waliotumia vidonge vya uzazi wa mpango (POPs & COCs) na wale waliotumia njia za  uzazi wa mpango zisizo na homoni.

Kati ya haya makundi matatu, wachunguzi walilinganisha majibu ya wanawake wenye mazingira mazuri na yenye afya ya uke (uke uliozungukwa na bakteria walinzi waitwao Lactobacillus morphotypes na pasipo na bakteria wa magonjwa ya uke) na wanawake wenye mazingira mabaya ya uke na wenye maambukizi ya bakteria, fangasi au vimelea vingine vya magonjwa.

Timu ya uchunguzi ikaangalia na kugundua wanawake wanakunywa vidonge vya uzazi wa mpango na wale wanaochoma sindano za uzazi wa mpango wako katika hatari ya mabadiliko ya kinga ya mwili hali inayoongeza hatari ya mtu kuambukizwa VVU kuliko wanawake wasiotumia njia za uzazi wa mpango wana hatari kubwa ya kuongezeka kwa mabadiliko ya kinga ya mwili na uwepo wa magonjwa katika uke huongeza zaidi hatari hiyo.

Kwa kuongezea, wanawake wenye maambukizi katika uke na waliokunywa vidonge vya uzazi wa mpango pia walikuwa katika hatari kubwa ya mabadiliko ya kinga ya mwili.

Kwa mfano mwanamke aliyekuwa na Hepesi (tutuko/malengelenge) ukeni aliyeamua kutumia sindano za uzazi wa mpango na mwanamke mwingine mwenye Hepesi ukeni aliyetumia vidonge vya uzazi wa mpango wote waliongeza uwezekano wa kuwa na kiwango kikubwa cha protini kinachovutia VVU kuingia kwenye seli.

"Wanawake wanapaswa kufahamu zaidi ili kufanya maamuzi na machaguo sahihi juu ya njia bora za uzazi wa mpango. Wanaume kwa wanawake wanapaswa kuelimishwa juu ya utafiti wetu, kwa kuwa wote wako katika hatari ya kuambukizwa, wanahitaji kuzuia na kutibu maambukizi" alieleza Dk. Fichorova. Aliiongezea,

Aliongeza kuwa "Matumaini yetu ni kuzuia madhara yasiyotakiwa ya njia za uzazi wa mpango zenye homoni zilizopo na kuboresha ili kuokoa mamilioni ya maisha kwa kutengeneza vyombo na mbinu mpya za kurejesha na kutunza hali ya afya ya mazingira ya uke kwa wanawake wote walio katika umri wa kuzaa"


Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Trending Articles