Quantcast
Channel: Afya – Fikra Pevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Ugonjwa wa kichomi waongoza kwa vifo miongoni mwa watoto Afrika

$
0
0

UGONJWA wa Kichomi umetanjwa kuwa ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababisha vifo vingi miongoni mwa watoto walio chini ya miaka mitano duniani, huku watototo zaidi ya milioni moja wakipoteza maisha kila mwaka kutokana na tatizo hilo katika maeneo mbalimbali barani Afrika.

Wakiongea na FikarPevu Julai 3, 2014 kwa nyakati tofauti madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali ya bidadamu katika Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Kilimanjaro, Kilimanjaro Christian Medical Centre (KCMC), (kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwenye mtandao) wamesema jamii inakabiliwa na tatizo la ukosefu wa elimu kwa kuwapeleka watoto wenye umri mdogo katika vituo vya afya kwa kujijengea tabia ya kuwatibu wenyewe majumbani na pindi tatizo linapokuwa kubwa hukimbilia hospitalini.

Mmoja wa madaktari hao (ambaye hakutaka jina lake litajwe kwenye mtandao) amesema,“hili ni tatizo kubwa nchini na barani Afrika kwa ujumla japo kuwa watu wanaliona kuwa la kawaida, ila kimsingi watoto walio na umri wa kati ya wiki tano hadi mwaka mmoja wanatakiwa wapelekwe kwenye vituo vya afya, ili wapate chanjo ambazo zitawakinga na magonjwa yanayosababishwa na ugonjwa huu”.

Amesisitiza kuwa jamii inatakiwa kubadilika na kutambua kwamba watoto wadogo wanatakiwa kupata chanjo za kinga ya magonjwa tofauti, ikiwemo kinga ya Donda Koo, Polio, Kichomi, Surua Pepopunda, Homa ya Ini, na Kifua Kikuu, na Uti wa Mgongo.

“Vifo vingi kwa watoto vinatokana na ugonjwa huu, na pia ugonjwa huu unaweza kuzuilika endapo tu kwa upande wa watoto wadogo watapata matibabu ya awali mapema, kwamaana ugonjwa huu pia unasababisha ugonjwa wa moyo kwa watu wazima na ambapo hii inatokana nakupatwa na kichomi kwa muda mrefu pia hata wakati ukitembea au ukishafanya mazoezi makali” alikaririwa mmoja wa daktari hao.

Taarifa kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, zinasema kuwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano wapatao 14,123 nchini, wamepoteza maisha mwaka 2012 baada ya kuugua ugonjwa wa vichomi.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>