Quantcast
Channel: Afya – Fikra Pevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Unyonyeshaji ni njia ya Uzazi wa Mpango, Maziwa ya mwanzo ya Mama ni muhimu kwa Mtoto

$
0
0

WANAWAKE wametakiwa kuwanyonyesha watoto wao kwa kipindi cha miezi sita mfululizo bila kuwapatia chakula chochote kingine ili wawe na afya bora pamoja na kuwakinga na magonjwa.

Kumnyonyesha mtoto kwa kipindi hicho kumetajwa  kuwa njia mojawapo ya uzazi wa mpango kutokana na kuzalishwa kwa homoni zinazozuia yai la mama lisipevuke.

Mratibu wa Huduma ya Afya ya Uzazi, Mama na Mtoto wa  Halmshauri ya Jiji la Mbeya, Nginael Ngowo, alisema hayo hivi karibuni alipokuwa akizungumza na mwandishi wa habari hii.

Alisema kuwa kuna baadhi ya wanawake  huacha mapema kuwanyonyesha watoto mara baada ya kujifungua kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo ya kuzidiwa na kazi.

''Mtoto anapozaliwa tu anatakiwa akae kwenye ziwa la mama ndani ya saa moja moja baada ya hapo mama anashauriwa kumnyonyesha ndani ya muda wa
miezi sita mfulululizo bila kumpatia kitu kingine hii itasaidia kukua vizuri kiafya na kiakili'' alisema.

Alisema kumuachisha mapema mtoto kunyonya kunaweza kukamsababishia magonjwa ya kuharisha na unyafuzi pamoja na kupunguza mahusiano mazuri kati ya mama na mtoto.

“Maziwa ya mama yana virutubisho na kinga ambazo zinamsaidia mtoto asipate magonjwa mbalimbali sambamba na kumfanya mtoto awe na akili timamu, pia kunyonyesha mfululizo ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango ambapo yai la mama huzuiwa kupevuka”, alisema.

Alishauri akina mama kuhakikisha kuwa wanawanyonyesha watoto kwa muda wa miaka miwili kutokana na umuhimu wa maziwa ya mama.

Daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Wazazi (Meta) iliyopo Mbeya, Elias Kaminyoge alisema kuwa njia ya unyonyeshaji kwa mfululizo kwa mama husaidia kwa asilimia kubwa mama kutopata mimba kwa kipindi cha miezi sita ya kwanza mara baada ya kujifungua.

“Kuna kitu kinaitwa ‘prolactin homon’ kwa kawaida mama anapokuwa ananyonyesha homoni hii huwa juu ambayo huwezesha maziwa ya mama kutoka, wakati huo huo homoni hii hufanya  mayai yasipevuke, hivyo kumfanya mama asipate hedhi kwa miezi sita ya mwanzo baada ya kujifungua”, alisema Dk.Kaminyoge.

Aidha, alisema njia hiyo inafanikiwa tu iwapo mama atanyonyesha mtoto wake muda wote pasipo kutoka nyumbani, vinginevyo uwezekano wa kupata mimba ni mkubwa, hivyo amewataka akina mama kutumia njia nyingine za uzazi wa mpango kwa usalama wa afya ya mama na mtoto.

Alizitaja baadhi ya njia nyingine za uzazi wa mpango kuwa ni kwa kutumia njia ya asili ya kutazama mabadiliko ya mwanamke, njia ya uwekaji wa kitanzi, vijiti, vidonge pamoja na kuchoma sindano.

Kwa mujibu wa  pima kadi (Scorecard) ya robo ya mwisho kwa mwaka 2014 katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, inaonyesha kuwa kati ya akina mama wenye umri kuanzia miaka 15 hadi 45,  ni asilimia 36 tu ndio wanaotumia uzazi wa mpango wa muda mfupi wakati asilimia 28 wakitumia uzazi wa mpango wa muda mrefu.
 


Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>