Quantcast
Channel: Afya – Fikra Pevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Upo uwezekano wa Mama mwenye VVU kufurahia Maisha ya kupata Mtoto bila Maambukizi?

$
0
0

WATAALAMU wa afya wanathibitisha kwamba kuna uwezekano mkubwa wa Mama mjamzito mwenye virusi vya Ukiwmi kujifungua mtoto asiye na maambukizi hayo.

Tunawezaje kuondoa hali hii ili kina mama wote wanaoishi na virusi vya Ukimwi wayafurahie maisha ya kupata watoto wasio na virusi vya Ukimwi?

Wafanyakazi wa sekta ya afya, watunga sera na mameneja wa programu wanaoshiriki kwenye shughuli za kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, wameithibitishia FikraPevu kwamba katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na changamoto ya kutokuwepo kwa dawa kwenye vituo vya afya kuhudumia walengwa.

Kwa mujibu wa Meneja wa Programu Kitengo cha Kuzuia Maambukizi vya Virusi Vya Ukimwi, kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT), Jijini Dar es Salaam, aliyejitambulisha kwa jina la Victoria Maheri, ameeleza kuwa jitihada za mfumo huo zinaweza kupunguza viwango vya maambukizi hadi chini ya 5% iwapo wanawake wajawazito na watoto wao wanapata na kushiriki kikamilifu kwenye huduma za PMTCT.

Aidha, amesema kwa sasa karibu 93% ya vituo vya afya nchini vyenye huduma za mama na mtoto (RCH) hutoa huduma za PMTCT1 na kuwa asilimia 98% ya wanawake wajawazito wanahudhuria kliniki za mama wajawazito angalau mara moja wakati karibu asilimia 43% wanahudhuria mara 4 kwenye kliniki ya maambukizi ya virusi vya Ukimwi wakati wa ujauzito wao.

Kwa mujibu wa tafiti kutoka Kitengo cha Kuzuia Maambukizi vya Virusi Vya Ukimwi, kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto (PMTCT), Jijini Dar es Salaam kuna vipindi vitatu ambavyo Mama mwenye virusi vya UKIWMI, anaweza kumuambukiza mtoto wake.

Kipindi cha kwanza ni kipindi cha ujauzito ambapo tafiti zinaonyesha kuwa, katika wanawake 100 wenye Virusi vya Ukimwi 5 hadi 100 kati yao wanaweza kuambukizwa virusi vya Ukimwi watoto wao.

Kipindi cha pili ni wakati wa kujifungua, ambapo wanawake 10-15 kati ya 100 wanaweza kuambukiza watoto wao.

Kipindi cha tatu nai kipindi cha kunyonyesha ambapo wanawake 10-25 wanaweza kuambukiza watoto wao lakini yote hayo yanaweza kutokea ikiwa tu akina mama hao hawakupata huduma za kuzuia virusi vya Ukimwi kutoka kwa Mama kwenda kwa Mtoto.

Hapa nchini, hadi kufikia mwaka jana, maambukizi hayo kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto ni wanawake 15 kati ya 100 lakini lengo la Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ni kupunguza hadi kufikia wanawake 4 hati ya 100 ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Baadhi ya waathirika wa ugonjwa huo, (hawakupenda kutajwa majina yao) wanasema wamewahi kwenda kuchukua dawa kila mara na hata baada ya kubeba mimba bila kuchelewa kuchukua dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo ili waweze kufurahia maisha ya familia zao.

Mmoja wa akina mama hao (36) anasema wakati akiwa mjamzito alikuwa anahudhuria kliniki yake ya dawa pamoja na kliniki ya mtoto ya ujauzito na Mungu alimsaidia hadi akajifungua salama na mtoto wake ameendelea kuwa mzima na baada ya kuona uchungu alienda hospitali na kuhudumiwa vizuri sana.

“Nilipofika na kuwaonyesha kadi yangu ya Kliniki, walisema huyu mtu anatakiwa kujifungua kwa usalama zaidi, ndio wakawa wamenisimamia na nikawa nimejifungua salama mtoto wangu ni mzima, baada ya wiki mbili nilimpeleka Muhimbili na kupimwa tukafuata majibu baada ya mwezi mmoja ikaonekana mtoto ni mzima” alieleza mmoja wa akina mama Jijini Dar es Salaam.

AfyaYasinta Lazaro (28) mkazi wa Kiwalani Jijini humo, amesema kukosekana kwa vipimo vya watu walioathirika na ugonjwa huo katika Zahanati wanazohudumiwa wakiwa wajawazito, kunawapa hofu ya kujifungua salama mara kadhaa na kuwa uwepo wa vipimo na dawa vina mchango mkubwa wa matokeo wanayoyapata.

Baadhi ya wahojiwa wamesema walikuwa hawajui kuwa wameathirika. Mmoja wa waathirika wa hali hiyo, amesema baada ya ujauzito wa kwanza hadi wa tatu kuharibika kwa kuwa alikuwa akiishi kijijini lakini kwa sasa amepata huduma za ushauri nasaha juu ya kitu anachopaswa kukifanya baada ya mimba kutunga.

Wakazi wa mkoa wa Tabora, wamesema vituo vingi vya afya havijafikiwa na huduma hiyo, huku wakiitaka Serikali kutoa mwongozo kwa wakuu wa vituo vya afya waweze kuwapa rufaa akina mama wajawazito ili waende kwenye vituo ambavyo vinatoa huduma kwa waathirika.

Pia wametaka waganga wakuu wa wilaya kuuliza kwenye vituo vya afya chini mapema ili kama kuna dawa zilizobaki ziweze kutumika kwa wagonjwa wengine ambao hawapati huduma hiyo.

Mfamasia na Mratibu wa Masuala ya Uagizaji na Upatikanaji wa Dawa katika Hospitali ya Wilaya ya Misungwi, Angela Kimaro, amesema kwa utaratibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wanawake wajawazito wenye maambukizi wanahitaji kupewa uangalizi wa juu ikiwemo kuwepo kwa vitendea kazi hospitalini ili viweze kutumika kutolea huduma.

Mratibu wa Mwenendo na Tathmini ya PMPCT, Dk. Prosper Njau, anasema ili kufanikiwa katika jambo lolote, lazima mfumo uboreshwe ili uweze kuleta dhana ya uwajibikaji.

“Kuhudhuria kliniki ya uzazi na kupima mimba ni huduma muhimu ambapo wafanyakazi wa afya, manesi na madaktari wanampima mama na kumfuatilia ili kuyazuia matatizo yanayojitokeza wakati wa mimba, kuyatambua na kuyatibu mapema.  Kwa kupima na kufuatilia mimba kutoka inapotungwa mpaka mtoto anapozaliwa kunazuia na kupunguza matatizo yanayoweza kutokea kwa mama na mtoto wakati wa mimba, wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua” alieleza Dk. Njau.

Hata hivyo, anasema miongoni mwa wanawake wajawazito waliobainishwa kuwa wameathirika na VVU na ambao wanapata kinga za ARV, karibu 63% wanapata mseto wa kinga ya ARV, 19% wapo katika matibabu ya ARV na 18% katika dozi moja ya Nevirapine22

Kujifungua kwenye hali ya usafi na pahala ambapo kuna huduma ya daktari au nesi kunapunguza uwezekano wa kupata matatizo wakati wa kujifungua yaani matatizo kwa mama na kwa mtoto.

Inapunguza uwezekano wa kudhurika mama au mtoto, mama akijifungulia nyumbani, akijifungulia mahali ambapo siyo pasafi, panapokosekana vifaa muhimu na wataalamu yaani daktari au nesi, mama na mtoto wana uwezekano wa kupata madhara ya kuumia na kupata maambukizi ya bakteria, virusi au fangasi.

Nusu ya mama wanaojifungua nchini yaani asilimia 50% hujifungulia kwenye kituo cha huduma za afya yaani hospitali, kituo cha afya au zahanati na nusu yaani 50% huzalia nyumbani.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Trending Articles