Quantcast
Channel: Afya – Fikra Pevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Gari la kubeba wagonjwa latumika kuneemesha watumishi wa afya Kahama

$
0
0

BAADHI ya Wananchi katika Kijiji cha Shunu katika Kata ya Nyahanga Wilayani Kahama mkoani Shinyanga, wamelalamika hatua ya kutozwa gharama ya shilingi 40,000 hadi 60,000 ya usafiri wa gari la wagonjwa (Ambulance) pindi wanapokuwa na wagonjwa wanaohitajika kwenda kupata matibabu zaidi kwenye Hopitali ya  Rufaa ya mkoa huo.

Taarifa zilizoifikia FikraPevu zinaeleza kuwa hali hiyo husababisha baadhi ya wagonjwa kupoteza maisha wakati wakiwa njiani kuelekea Hospitalini baada ya kukosa fedha hizo na kuwa akina mama wajawazito ndio wanaoathiriwa zaidi na suala hilo ambapo imedaiwa mara kadhaa kuzalia majumbani au njiani.

Wakiongea kwa nyakati tofauti mara baada ya Mama mmoja mjamzito aliyenusurika kifo baada ya ndugu wa mgonjwa kukosa fedha za kugharimia fedha hizo ambapo wamesema wamekuwa wakitozwa kiasi hicho na uongozi wa Hospitali ya wilaya hiyo.

“Pamoja na kuwa ukiwa na shida huwezi kujali gharama au vyovyote lakini hili limetuchosha kwamaana wananchi wengine hatuna uwezo ndio chanzo cha Mama mmoja wiki mbili zilizopita kunusurika kufa baada ya kukosekana kwa fedha hizo kwamaana alijifungua salama lakini hatuwezi kuishi hivi kwamaana serikali ilisema lile gari halitakiwi kukodishwa lakini wenzetu wamefanya kitega uchumi”.

Naye Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Shunu, Benjamin Makelo, amesema licha ya wananchi kupewa elimu ya kujiandaa kumpokea mtoto kwa mama mjamzito gari hilo limetolewa na serikali kwa matumizi ya rufaa pekee na kuwa wagonjwa wanatakiwa kusafirishwa bure kama yalivyo maagizo ya serikali na kuwa mtu atakayetoa toa fedha atakua ametoa kwa hiari yake.

“Hili tatizo tushawaambia wananchi kuwa mafuta yatakuwepo kila wakati ila wagonjwa watakao hitajika zaidi kutumia ile gari la wagonjwa ni mama wajawazito walioshindwa kujifungua waliopata ajali na wagonjwa mahututi” alikaririrwa akizungumza na FikraPevu.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Benson Mpesya, amesema huduma ya gari la wagonjwa ni bure wala hakuna ruhusa ya kutoa fedha ya aina yoyote, huku akiwahakikishia wananchi waliokutana na adha hiyo kuwa suala la upatikanaji wa mafuta kwenye gari hilo utakuwepo hivyo wananchi wasiwe na hofu juu ya hilo.

Katika hatua nyingine Mpesya, amewataka wananchi walioshawishiwa na watumishi wa Hospitali hiyo kutoa taarifa ya katika Ofisi yake ili wahusika waweze kuchukuliwa sheria stahiki.

Kumbukumbu zinaonyesha kuwa haya yanatokea wakati katika maeneo mbalimbali nchini, magari ya kubeba wagonjwa yakikamatwa katika maeneo hayo yakifanya shughuli za watu binafsi ikiwemo kutumika kwa ajili ya kufanya uhalifu bila wahusika kuchukuliwa hatua stahiki.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Latest Images

Trending Articles

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>