Quantcast
Channel: Afya – Fikra Pevu
Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

‘Thamini Uhai’ yaokoa maisha ya mama mjamzito

$
0
0

KAMPENI ya 'Thamini Uhai, okoa maisha ya mama mjamzito na mtoto' inayoendeshwa na Shirika lisilo la kiserikali la World Lung Foundation Tanzania (WLF) chini ya ufadhili wa Swedish Internatinol Agency (SIDA) imesaidia kuondoa tamaduni na tabia ambazo zinapelekea matumizi madogo ya vituo vya huduma za afya wakati wa ujauzito.

Taarifa ya shirika hilo (FikraPevu imepata nakala) inasema, Oliva Tryphone, mkazi wa kijiji kimoja cha mbali nchini (haikueleza ni Kijiji gani, Wilaya wala Mkoa) amenusurika kufa wakati akiwa mjamzito katika siku za hivi karibuni na kwamba jambo lililomhamasisha kufanya maamuzi ya kujifungulia hospitalini ni kampeni inayoendeshwa na shirika hilo kupitia matangazo yake yanayorushwa na radio zilizopo nchini licha ya jamii yake kuwa na utamaduni wa kujifungulia majumbani.

Wauguzi katika hospitali hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mzazi huyo, ambaye aliyejifungua kwa njia ya oparesheni

Wauguzi katika hospitali hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mzazi huyo, ambaye aliyejifungua kwa njia ya oparesheni

Aidha, taarifa hiyo inaeleza kuwa katika kijiji anachotoka mwanamke huyo, jamii inakasumba ya kujifungulia majumbani na kwamba mara baada ya kuwasili katika hospitali aliyojifungulia wataalamu wa afya waligundua kuwa hawezi kujifungua katika njia ya kawaida hadi afanyiwe oparesheni.

Mwanamke huyo chini wa uangalizi wa madaktari hao alijifungua mtoto mwenye uzito wa 2.8kg na kwamba mtoto alikuwa amechoka hali iliyowalazimu madaktari kumuweka hewa (oxygen). Hali ya mama na mtoto kwa hivi sasa inaelezwa kuwa inaendelea kuboreka na kuwa wameruhusiwa kwenda nyumbani Octoba 28, 2014 huku akitakiwa kurudi baada ya siku saba.

Wauguzi katika hospitali hiyo wakiwa katika picha ya pamoja na mzazi huyo, ambaye aliyejifungua kwa njia ya oparesheni 01

Tafiti zinaonyesha kuwa moja ya sababu zinazotajwa kuchangia tatizo hilo inajumuisha fikra potofu kuhusiana na usalama wa kujifungua nyumbani, ukosefu wa mpango binafsi wa kujifungua, kujua umbali mrefu na suala la usafiri ambalo akina mama wengi wanakabiliana nalo katika kufikia vituo vya huduma za afya na wakati mwingine inajumuisha uwezo mdogo na uangalizi duni katika vituo vya afya.

Moja ya lengo la kampeni hiyo ni pamoja na kuhamasisha jamii katika kuongeza juhudi za kuboresha huduma bora za kiafya kwa mama wajawazito wakati wa kujifungua.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 296

Trending Articles



<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>